Saturday, January 7, 2012

Umri wako ni deni

Siku zako zote deni, ukifika utu uzima,
Ifanye na tathmini, kuzilipa ni lazima,
Urushi ndani huoni, mkopwaji ni Karima,
Umri wako ni deni, tena lazima kulipa!

Haya ukiyabaini, maisha umeazima,
Utakuwa ni makini, kumwogopa Rahima,
IMF wao ni nini, waiga yake hekima,
Umri wako ni deni, tena lazima kulipa!

Atayafuta madeni, ya mbele hata ya nyuma,
Ipande yako mizani, kwa faida na heshima,
Akhera na duniani, uwe nawe muadhama,
Umri wako ni deni, tena lazima kulipa!

No comments: