Thursday, January 12, 2012

Ujanja unapozidi,

Ujanja ukishajaa, akili zinapungua,
Ndivyo inavyotokea, wajanja wakizaliwa,
Na watu wakashangaa, kwa yanayowatokea,
Ujanja unapozidi, akili zinapungua.

Ujanja wa kushupaa, akili kazi kukua,
Palepalel hubakia, zisiache zungukia,
Hujua wanayojua, hawajuui wasojua,
Ujanja unapozidi, akili zinapungua.

Hoja zao hujavia, wakabaki kuzomea,
Akili zinazochanua, maji zije kuzuiwa,
Na mbegu ukizisia, aghalabu huzing'oa,
Ujanja unapozidi, akili zinapungua.

Akili yao huwa njaa, starehe nazo raha,
Si watu wa kutambua, na muda kujipangia,
Huvuna wasiposia, na majangwa kuyazua,
Ujanja unapozidi, akili zinapungua.

No comments: