Thursday, January 12, 2012

Choo hakina mkubwa

Choo mkubwa hakina, budi wote kutumia,
Vipi mwenzangu wanuna, kwa wengine kutumia ?
Hili halina utwana, wote hapa watu sawa,
Choo hakina mkubwa, hata wadogo wajibu!

Tumbo kitu cha amana, na wote tumegaiwa,
Vitu vinapopishana, husagwa na kutumiwa,
Ila visivyofanana, ni lazima kuachiwa,
Choo hakina mkubwa, hata wadogo wajibu!

Ila visivyofanana, ni lazima kuachiwa,
Ndipo hapo twashindana, chooni kukimbilia,
Nafuu mtu kuona, kawaida kurejea,
Choo hakina mkubwa, hata wadogo wajibu!

Usiwe nayo hiana, choo kukitumia,
Yatakupata mtwana, utakayoyajutia,
Ukakosa muungwana, hata wa kukusaidia,
Choo hakina mkubwa, hata wadogo wajibu!

No comments: