Thursday, January 12, 2012

Nchi ikikosa maji

Nani wa kulaumiwa, kwa miji siyo na maji,
Nini kilichotokea, mpaka leo wafujaji,
Mkenge tulipoingia, ni wa njaa au ulaji?
Nchi ikikosa maji, nani wa kulaumiwa?

Rugemalila mwajua, cha kwanza chuo cha maji,
Ni nini kimetoa, na wapi chaenda hiji?
Au ni maghofu yawa, tabia ya wauaji?
Nchi ikikosa maji, nani wa kulaumiwa?

Programu yakufaa, ipi tunayotaraji,
Au yafa historia, moja kuanza twahoji,
Hili kweli tutakua, kama huu ni mtaji?
Nchi ikikosa maji, nani wa kulaumiwa?

Nani wa kuwaambia, hawa wetu wenye mjia,
Hiki kinachotokea, ni akili za saruji,
Kuganda zimezoea, na mwishowe ni Kimbiji,
Nchi ikikosa maji, nani wa kulaumiwa?

No comments: