Thursday, January 12, 2012

Hali ya hewa ni mbaya

Si mimi watakwambia, hewa wanaochafua,
Wapi utakapokaa, ukweli ukaujua,
Wengine wamesomea, watu kuwahadaa?
Hali ya hewa ni mbaya, ni nani kaichafua ?

Si nje aliyekaa, ndani naye tumekaa,
Si mgeni nakwambia, ni mwenzetu alokuwa,
Na karibu katulia, yuusuffu amtumia,
Hali ya hewa ni mbaya, ni nani kaichafua ?

Astaghafirullahi natoa, kwa huyo kumdhania,
Wenyewe tunajijua, kula tulichojaliwa,
Matumbo yakikataa, hivyo ndivyo inavyokua,
Hali ya hewa ni mbaya, ni nani kaichafua ?

Marashi nimetumia, na hayajasaidia,
Ninazidi lewalewa, puani hewa kwingia,
Najuta nilipokaa, hali siwezi sogea,
Hali ya hewa ni mbaya, ni nani kaichafua ?

No comments: