Thursday, January 12, 2012

Ndoto kuwa nazo

Ndoto kuwa nazo sawa, ila zifanyiwe kazi,
Maendeleo ni taa, huyamulika makazi,
Upate kuona njia, kwenda hata kwenye mwezi,
Ndoto kuwa nazo sawa, ila zifanyie kazi!

Ndoto kwako wewe taa, kufanya ni mazoezi,
Kila unapotembea, huongeza na ujuzi,
Unavyorudiarudia, ubingwa huja darizi,
Ndoto kuwa nazo sawa, ila zifanyie kazi!

Kitu ukishafikiria, anza kufanzia kazi,
Alinacha kutokuwa, ukalalal usingizi,
Mambo yataka hatua, za ujenzi na tatuzi,
Ndoto kuwa nazo sawa, ila zifanyie kazi!

Mwendo usipoanzia, huyafanzi mapinduzi,
Ndotoni utabakia, na kulewa usingizi,
Kama wataka ogelea, lazima kupiga mbizi,
Ndoto kuwa nazo sawa, ila zifanyie kazi!

Lawama kusingizia, hazinayo ufumbuzi,
Hubaki kulialia, wengine waacha njozi,
Na kileleni wakwaa, wewe kupanda huwezi,
Ndoto kuwa nazo sawa, ila zifanyie kazi!

No comments: