Thursday, January 12, 2012

Kinywa kukosa meno

Kinywa kikikosa meno, sio mwisho wa kuteta,
Ulimi huunda neno, kukosa meno si utata,
Pawapo msuguano, kwa pumzi hutakata,
Kinywa kukosa meno, sio mwisho wa kuteta!

Hauishi mshikamano, kwa meno kuyakeketa,
Hukosi maelewano, kama lazima kuteta,
Hauhitaji sindano, wala knywa maji lita,
Kinywa kukosa meno, sio mwisho wa kuteta!

Na hapana mabishano, na pia kusitasita,
Huwa safi mchuano, na mambo kumeremeta,
Huweka lake agano, kusije isha kuteta,
Kinywa kukosa meno, sio mwisho wa kuteta!

Nimeleta mlingano, kauli hii kuteta,
Na wala sio ndoano, samaki kuwakamata,
Ali na wewe Machano, muache kunitafuta,
Kinywa kukosa meno, sio mwisho wa kuteta!

No comments: