Thursday, January 12, 2012

Bora kulemaa mwili, kulikoni kiakili!

Bora mwili kulemaa, kulikoni ukichaa,
Ukawa unatembea, ufanyalo kutojua,
Ninaomba sana dua, hili nikaepushiwa,
Bora kulemaa mwili, kulikoni kiakili!

Akili ikilemaa, nini utafikiria,
Utumwani huishia, wengine kutumikia,
Na kisha kuwa kinyaa, jalalani kuishia,
Bora kulemaa mwili, kulikoni kiakili!

Na wengi waliokua, siasa wanaingia,
Hii ni yato tabia, watumwa kuwatumia,
Rijali waliokuwa, sinema wao wakawa,
Bora kulemaa mwili, kulikoni kiakili!

Ukubwa waliopewa, makuwadi huja kuwa,
Au uboi hupewa, mabwana kuwatumia,
Ndio maana husinzia, hata bungeni wakiwa,
Bora kulemaa mwili, kulikoni kiakili!

No comments: