Thursday, January 12, 2012

Ndoa ya Mwafrika na mzungu

Leo nazua umbeya, ninataka kuambiwa,
Mwafrika akioa, mweusi asiyekuwa,
Mathalani kumvaa, Mzungu aliyekuwa,
Mzungu na Mwafrika, ndoayo nani apata?

Ni nani anapatiya, Mzungu ukimuoa?
Afaidia kwa hatua, kuliko inavyokua,
Utafiti unafaa, kuanza kujifanyia?
Mzungu na Mwafrika, ndoayo nani apata?

Hili ningelilijua, ushauri ningetoa,
Kama sasa inafaa, utandawazi kusambaa,
Hadi China kuingia, nako Malaysia pia,
Mzungu na Mwafrika, ndoayo nani apata?

No comments: