Tuesday, January 10, 2012

Utungo huu wosia

Utungo huu wosia,
Wanangu nawaachia,
NInamuomba Alaa,
Ukubwani kuwafaa.

Dunia ikijakubakia
kwa ajili yako,
wewe hautobakia
kwa ajili ya dunia!

Mashehe wamenambia,
Na mimi kuaminia,
Lipi la kuulizia,
Ukweli uliokua?

Dunia ikijakubakia
kwa ajili yako,
wewe hautobakia
kwa ajili ya dunia!

Na nilichokigungua,
Muda mfupi twapewa,
Kukaa kwenye dunia,
Na kifo kikawadia,

Dunia ikijakubakia
kwa ajili yako,
wewe hautobakia
kwa ajili ya dunia!

Ujana hutuhadaa,
Milele tukadhania,
Kuishi tutajaliwa,
Na siku kuzingojea.

Dunia ikijakubakia
kwa ajili yako,
wewe hautobakia
kwa ajili ya dunia!

Tukijakushtukia,
UZee unaingia,
Nguvu zikatuishia,
Kusali tukalemaa.

Dunia ikijakubakia
kwa ajili yako,
wewe hautobakia
kwa ajili ya dunia!

No comments: