Mifuko wanachukua, michango wasiotoa,
Wanachama wabakia, kila siku wana njaa,
Na miradi yasambaa, mikubwa iliyokua,
Hisa NSSF, kwanini nakataliwa?
Mashirika mmeua, ya uma iliyokuwa,
Wenzetu mmejaliwa, ujira ni wa Ulaya,
Bongo tunaolipiwa, kidogo mnakitukua,
Hisa GEPF, kwanini nakataliwa?
Hela tunaulizia, wapi mlipozitia,
Mashirika mwajiuzia, na wengine wachukua,
Sisi hata kutugeea, hisa kazi inakuwa?
Hisa PPF, kwanini nakataliwa?
Serikali ilitia, kipi kilichowanyanyua,
Kama si michango yawa, hii sisi tunayotoa?
Halafu haramu yawa, kwa riba kutugaia?
Hisa LAPF, kwanini nakataliwa?
Twataka hisa chukua, kama dini mwaijua,
Madhambi kuyaambaa, mgawo tukapokea,
Na akhera na dunia, tusiwe cha kujutia,
Hisa mifuko mingine, kwanini nakataliwa?
Tuesday, January 10, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment