Thursday, January 12, 2012

Ubinafsi wa kuua,

Ubinafsi waua, lazima hili kujua,
Na hapo ikifikia, muuaji huuawa,
Sio lazima kuioa, rohoye moya kwa moya,
Ubinafsi wa kuua, adhabu yake ni kifo.

Miradi wanaouwa, wengi inayowafaa,
Hawa sawa wamekua, wauaji wa kudhamiria,
Kitanzi kinawafaa, au risadi kutia,
Ubinafsi wa kuua, adhabu yake ni kifo.

Twachoka wavumilia, nchi inadidimia,
Bila hatua kutwaa, watu watateketea,
Haya tukiyaridhia, hapana pa kusimamia,
Ubinafsi wa kuua, adhabu yake ni kifo.

Neno nimeshawaambia, na mwenyezi ndiye mjua,
Haya mkiyatania, mtakuja yachambia,
Kila mtua atajua, mwana mlivyoshamlea,
Ubinafsi wa kuua, adhabu yake ni kifo.

No comments: