Imewakuta mipasho, ulaji kuwa ulwaji,
Kwa wengine kichekesho, mchuzi kufanywa uji,
Waupata mchemsho, kukiongeza kilaji,
Ni ulaji na ulaji, josho limekuwa jasho.
Mkuu kafanya sitisho, kayaona mauaji,
Yake wala si vitisho, kawavaa wajuaji,
Nchi sio mchemsho, kila mtu kujifafriji,
Ni ulaji na ulaji, josho limekuwa jasho.
Josho limekua jasho, nani mtetemekaji,
Muosha wake muosho, mbona sasa haukuji,
Tubange kama korosho, kwenye miji na vijiji,
Ni ulaji na ulaji, josho limekuwa jasho.
Yafaa maibisho, pamwe na uburuzaji,
Ngosha ataka makosho, wala hangoji majaji,
Yaanzayo yana mwisho, yaende kwenye friji,
Ni ulaji na ulaji, josho limekuwa jasho.
Thursday, January 12, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment