Mwanasesere kongoza, midoli mtageuzwa,
Mzungu kazungumza, Mwafrika ataweza ?
Na kinachotumaliza, sanaa na kuigiza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Heri kiumbe kumezwa, kulikoni kulemazwa,
Akili kutekeza, nyani mtu kugeuzwa,
Iwe huna unaloweza, isipokua kuigiza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Mwanasesere kaiza, kazi hii fungameza,
Mbwani mwapatiliza, pamoja kupitiliza,
Njiani asiyeuliza, mdudu humpoteza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Mwanasesere kaviza, mchezo hataki cheza,
Kila ukimtengeza, azidi kujitatiza,
Na hao wanaomcheza, vingine hawataweza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Kusema sijamaliza, mbona mnajiingiza?
Neno mnaligeuza, mbona mnapandikiza?
Mtunzi sijaangaza, nyie mwaona mwangaza?
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Uongozi sio kwanza, wala wa kutanguliza,
Juu mwaweza wakweza, wezi wakawamaliza,
Na nchi kuteketeza, kama vile wanacheza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Kazi niliyoianza, bado sijaimaliza,
Na siwezi kumaliza, kwani siwezi igiza,
Wajao nawaeleza, anzeni kuendeleza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Nchi imenichakaza, na akili kuburuza,
Wajuu wananikwaza, vipi nije kuwafunza,
Unafsi watanguliza,atawajaza Muweza,
Mwanasesere kaiza, leo na nani twacheza?
Unapendeza uoza, kwa juu walio kwanza,
Ukitaka tengeneza, katu hawatasikiza,
Nchi imekengeuzwa, wabaki kuimaliza,
Tuesday, December 13, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment