Wednesday, December 14, 2011

Usenge ubaki kwenu

Usenge hidaya yenu, Ulaya nayo kaeni,
Afrika sio kwenu, hayo kwetu ya kigeni,
Tumtwange kwenye kinu, ajae kutuzaini,
Usenge ubaki kwenu, muiache yetu imani!

Na sisi sio wenzenu, Clinton na Marekani,
Sodomu muite kwenu, sisi hapa abadani,
Twazisikia fununu, mwatutaka tuamini,
Usenge ubaki kwenu, muiache yetu imani!

Gomorah ni radhi yenu, kwalo hatuna utani,
Bakini na hivyo vyenu, ya kwetu tuachieni,
Kama ni CCM na TANU, hao wawe wenu watani,
Usenge ubaki kwenu, muiache yetu imani!

Mnawajua wenzenu, kuwafata masikani,
Tulishaamba si tununu, hatufai Marekani,
Wakajitia ni nunu, binti wapenda wahuni,
Usenge ubaki kwenu, muiache yetu imani!

Hii sio yetu tunu, ni ya kwenu jamani,
Muitumie na kinu, kusaga yaso thamani,
Mwisho wetu sio wenu, na haiwi asilani,
Usenge ubaki kwenu, muiache yetu imani!

No comments: