Friday, December 16, 2011

Hujaumia hujaumbika

Hujafa hujaumbika,
Wahenga walitamka.
Uipatapo ajali,
Ndipo hili huwa kweli.

Wakubwa wanaokua,
kushuka hawajajua.
Ila siku ikifika,
ndipo wanaerevuka.

Tajiri wanaokua,
ufakiri husikia.
Ila wakifilisika,
ukat ahueleweka.

Tungo mpya 2011
Aina: Nanenne
© 2011 Sammy Makilla

No comments: