Friday, December 16, 2011

Waliokwishapotea

1.
Anapowahurumia, walokwishachaguliwa,
Rehema huwashukia, huruma zikawaingia,
Na pale wanapojijua, utu kwao hurejea,
Baraka huteremshiwa, sumu yao kuwa dawa,
Maafa kuwa manufaa, na ufisadi kuwa faida,
Kila kitu wakitwaa, mara dhahabu inakuwa,
Dunia ikashangaa, ibilisi kumkataa,
Mola kumgeukia, na wauwe kutumikia,
Waliokwishapotea, Mwenyezi anapopenda,
huja dhambi kutubia!


2.
Ila shetani akiwa, ndio anawasimamia,
Hawawezi kujijua, udhalimu huwavaa,
Waone wahusudiwa, wengine wana tamaa,
Musuli kuziumua, na ujibari kunoa,
Mapanga wakatumia, kama ilivyo Syria,
Wanyamaze wanaolia, kilio kutokusikia,
Ngozi ya kondoo walovaa, kuivua kukataa,
Kazi wakadhamiria, kawaida kuendelea,
Waliokwishapotea, Mwenyezi asipopenda,
moto wao hupalilia!!!

© 2011 Sammy Makilla

No comments: