Friday, December 16, 2011

Refutano hili hapa

Shairi nililowaandalia, refutano jina lateuliwa,
Ni kumi na moja latakiwia, mizani zake kuziangalia,
Na mistari inayotakiwa, yalazimu mitano kutimia,
Hapo ndipo utamu huingia,na refutano likakubaliwa,
Na ujumbe ukiuzingatia, shairi budi litakunyanyua!

Tungo mpya 2011
Aina: Refutano
© 2011 Sammy Makilla

No comments: