Friday, December 16, 2011

Kuua udugu

Kitu gani ndugu tunachokigombea,
Akhera kwenda nacho tukajajaliwa?
Ni jambo gani tunalolifikiria,
Udugu wetu tunaamua kuua?
Ni hizo mali tunazozikadiria,
au ni nyumba makaburi yasokuwa?

Ni kizazi klichokwisha kulaaniwa,
Udugu kinachothubutu kujaua,
Kizazi chake jua husambaratishwa,
Hatimaye lazima kitaangamia,
Hukipatiliza wakuabudiwa,
Kwani si kati ya anayoyaridhia.

Tungo mpya 2011
Aina: Misita
© 2011 Sammy Makilla

No comments: