Mweusi dhahabu fala, mweupe hufadhiliwa,
Mtawala naye hula, mweusi mgumu kutoa,
Ni goli mia kwa bila, nani kuja yakomboa?
Dhahabu mweusi fala, mweupe bure apewa!
Siasa zachakachua, bora tuliyojaliwa,
Manyanti tunshakua, kuiga yasiyofaa,
Njia hatujaijua, raia kuwanyanyua,
Dhahabu mweusi fala, mweupe bure apewa!
Misaada twapokea, tunazidi kufulia,
Kisirani chaingia, wenyewe twajishushua,
Kupendana kumevia, nafsi zatangulia,
Dhahabu mweusi fala, mweupe bure apewa!
Mweusi huwa kinyaa, mzungu kuthaminiwa,
Na Mchina kaingia, mambo vivyo yanakua,
Wengi ukiulizia, gea mbaya wakwambia,
Dhahabu mweusi fala, mweupe bure apewa!
Haijawa nchi kua, wengine kutegemea,
Hilo halijatokea, na wala haitakua,
Bure tunajisumbua, na muda unapotea,
Dhahabu mweusi fala, mweupe bure apewa!
Wednesday, December 14, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment