Asilimia mbili na nusu,
tisini na saba na nusu nini yawahusu?
Hata ndoa si tu mabusu,
Bali pia kudurusu
na mengine kukata kwa kisu,
Na kila linalotujusu
kizazi kipewe mpya libasu
Kupima ikakubali
au cha kale kukataa
na mbele kutawakali!
Ndoo wengine wenye njaa,
maamuzi wanayasifia,
Haya yasinelikuwa
wangelikuwa wadodea,
Cha bure wanakitumia
watunyima cha kununua?
Vyama walivyozua,
Nafasi zilikigombania,
Unguja kujipatia,
Bara mbali watupilia,
Ukweli tumeshaujua,
Wananchi tuliokiambiwa,
Ni Unguja na Pemba walokua,
Haikuwa Watanzania,
Wadanganyika
Watanganyika.
Nchi mbili moja huzaa
sio mbili tena kubakia
Hatua tuliyofikia,
Hata nayo mikoa yahjitajia,
Nchi thelathini zikawa,
hata ndogo zikiwa
Lakini zimeungania
Kuifanya Tanzania.
Tuanzie pa kuanzia,
Tanganyika kurejea,
Nchi mbili zenye ndoa
Zanzibar na Tanganyika
Kuienzi Tanzania
iwe kubwa Azania,
Waje kuingia pia,
Angola, Burundi, Malawi,
Msumbiji, Rwanda na Kongo pia.
Uganda na Kenya twajua,
Kaskazini zakimbilia,
Somalia wanachukua na
Sudan ya Kusini pia,
Chad wataendelea
Na Ethiopia kuingia,
Ni jeopolitikia mpya iliyokua,
na wachache wayajua haya!
Wednesday, December 14, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment