Hawezi kufilisika, dhahabu anayetwaa,
Roho ya nchi kashika, na wengi huwanunua,
Na kukopa husifika, hatamu vinavyokua,
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Wengine anayetaka, kuja kumhudumia,
MIpaka amepituka, ni bure awazawadia,
Mashimo yatachimbika, pasiwepo la kutia,
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Mitambo yaazimika, na 'lease' wanatoa,
Iweje twaambiwa, tumeshindwa kununua,
Na kuazima yafaa, na kazi kuendelea?
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Hicho mlichopokea, ndicho kinawazuzua,
Nchi mmeilangua, kukiri mwaona haya,
Yetu macho twaangalia, yaja tusiyoyajua,
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Wananchi wamesikia, kwingine yalikotokea,
Watu wameyakataa, na milki kubandua,
Batili imeshakua, mikataba walotia,
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Tanzania kutokea, ni wengi tutaumbua,
Waliojichukulia, cha mbele kilichokua,
Na kasri kuinua, na vidani kuvivaa,
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Matofali walopewa, orodha tunaijua,
Tutaka kujaambiwa, jinsi ilivyotokea,
Na hesabu kukagua, kama kweli zatimia,
Dhahabu anayeshika, huwa yeye mtawala!
Kodi kuziangalia, na wapi zilipoanzia,
Wapi zimeshaingia, na nini kimetufaa,
Pungufu kama ikiwa, ajua budi ikawa,
Wednesday, December 14, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment