Wednesday, December 14, 2011

Dhahabu si ya serikali

Dhahabu ya Watanzania, ndivyo ninavyotambua,
Haijawa haitakuwa, serikali kuchukua,
Kisha ikatuambia, kama hicho kisichokua,
Dhabau si ya serikali, ni mali ya Watanzania!

Dhahabu ilipokua, watu wake kuwafaa,
Vingine kuwaibia, neema mkachukua,
Wapaswa kujitetea, hilo linapotokea,
Dhabau si ya serikali, ni mali ya Watanzania!

Serikali yatakiwa, hili kuliangalia,
Mali wanayotakiwa, kumiliki ni raia,
Wahuni wakivamia, weza kuja kuuawa,
Dhabau si ya serikali, ni mali ya Watanzania!

Wageni wakivamia, weza kuja kuuawa,
Na walipwao fidia, vijijini walokua,
Mjini wakichukua, utapeli huja kua,
Dhabau si ya serikali, ni mali ya Watanzania!

Ni mali ya Watanzania, ndivyo ninavyotambua,
Utajiri watakiwa, mfukoni kuutia,
Na hisa kuzichukua, kwa kila wanaochimbua,
Dhabau si ya serikali, ni mali ya Watanzania!

No comments: