Afrika ina mchezo wa kuigiza
Tokea tupate uhuru ulianza
Na wakubwa waigizaji walioanza
Ni wale vita vya uhuru wasioongoza
Ila katikati walikujajitumbukiza
Viongozi wa kweli na haki wakawakwaza
Kisha wao wakaiba kujakuongoza.
Kiongozi wa kweli aghalabu huiza
Ni kwa muda mfupi tu angeliongoza
Kama Mzee Mandela alivyofanyiza
Wale ambao kazi yao ni kujikweza
Hao ni wanaizaya yao waendeleza
Uongozi hawatakaa waje kumaliza
Maana ni mradi wa madhambi kufanyiza
Na watu wao katu hawataendeleza
Sembuse nchi zao zenye maliwaza.
Na vyama vya kisiasa walivyovianza
Muumba vyote sasa keshavipatiliza
Vimekuwa hakika vyama vya kuigiza
Vingine mbali sana vimeshapitiliza
Vimeacha kuigiza, vinavyafanyiza:
' Demokrasi si serikali ya watu,
kwa ajili ya watu na inayoongozwa na watu!'
Bali wameigeuza sasa imekuwa ni:
' Demokrasi ni serikali ya wizi,
kwa ajili ya wizi na inayoongozwa na wezi!'
Na mchezo wanaendelea kuigiza
Maana watu wao wameshawapumbaza
Njaa na kiu kila siku vyawamaliza
Kuna wengine sasa wananunua giza
Gubigubi wananchi kuwafunikiza
Usingizi mchana na usiku kuwameza
Wasiweze watu wajinga kujitokeza
Waulize maswali kujibu yakawakwaza!
© 2011 Sammy Makilla
Friday, December 16, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment