Maamuzi huua, subira ikitoweka,
Hapana kufikiria, na mambo yanafanyika,
Hakuna kuangalia, na kupima kwafanyika
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Subira inatakiwa, vitabu vimeandika,
Hli sasa twashangaa, watu wanavyohangaika,
Imezidi yao haraka, katika kuamua,
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Wajinga washangilia, hawana la uhakika,
Ni ndia ya kutitia, iliyojaa mashaka,
Waamini kupitia, tena hawana wahaka,
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Mafuu utadhania, wanavyoweweseka,
Mauti yatangulia, nyuma wafatwa kuzikwa,
Na ndivyo inavyokua, kwa wanafiki mizuka,
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Uzazi usiojua, hatimaye si baraka,
Na wanachokitegemea, sicho kitakachotokea,
Chini huja kurejea, kila juu anayefika,
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Uchamungu waokoa, zipitazo hekaheka,
Ni maisha ya bandia,subira yasiyotaka,
Na mola hawajamjua, hao wanayoyataka,
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Watu wanapotutumia, na ubwege kuringia,
Maaluni hujifua, na hayawani tukawa,
Hakuna lakusikia, hadi tunaangamia,
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Kwingine twashuhudia, haya yanavyotokea,
Ila wajinga twabakia, kudhani tutaambaa,
Mafifa hatujatengua, hili kweli twalijua?
Subira ikitoweka, maamuzi huua.
Wednesday, December 14, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment