Waniuliza tatizo, mbona nazidi kuwaza,
Haulioni tangazo, kana kwamba watatiza,
Kama vile hamnazo, na si mtu wa kuwaza?
Nina msongo wa mawazo, kwayo unayonifanza!
Unapoondoa nguzo, kusimama sintoweza,
Unavunja mttelezo, nitaweza kuteleza,
Nikitoa maapizo, hadi mwisho utaweza?
Nina msongo wa mawazo, kwayo unayonifanza!
Mhemuko si mchezo, msongo unaukuza,
Nawe kwako ni igizo, mwanaizaya wayaweza,
Kwani sasa mjini gumzo,kila mtu aeleza,
Nina msongo wa mawazo, kwayo unayonifanza!
Na haya asiye nazo, ndiye haya huyaweza,
Umebakia shangazo, kiumbe hujajifunza,
Maisha kwako mzozo, utulivu hutoweza,
Nina msongo wa mawazo, kwayo unayonifanza!
Vipo vyuo vya mafunzo, na kusoma hukuweza,
Upewayo mahimizo, chuoni umeyasaza,
Yana mwisho yenye mwenzo, lazima utajifunza,
Nina msongo wa mawazo, kwayo unayonifanza!
Namuomba Muongozo, apate nielekeza,
Ipungue shinikizo, kazi zangu kuzifanza,
Ibada nazo nguzo, niweze kuzitimiza,
Nina msongo wa mawazo, kwayo unayonifanza!
Tuesday, March 6, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment