Saturday, March 24, 2012

Serikali kama wewe

Hadithi nimesikia, matajiri walokuwa,
Kipato hujipatia, sawasawa Tanzania,
Ndio kujiulizia, hivi kweli itakuwa?
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Kumbe huwa yatokea, tajiri mtu akawa,
Kuliko inavyokua, nchi anayetokea,
Na kisha kuisaidia, dhiki ikiishambulia,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Ujamaa Tanzania, watufanza kulemaa,
Wengi tuanvyodhania, tajiri huwezi kuwa,
Nchi ikakutegemea, nawe ukaisaidia,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Makopo tunachukua, serikali kufatia,
Msaada kupatiwa, hayo yetu mazoea,
Tuibadili tabia, hii ndiyo njema njia,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Mmoja tukianzia, fanya unachokijua,
Kizuri kikishakua, mali utajichumia,
Miradi tele yajaa, waa ni mkopo kupewa,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Vyama navyo pia, kazini viantakiwa,
Uchumi kwenda kulea, wakawekeze kwa nia,
Au makundi yakiwa, nao yanafadhiliwa,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Ukombozi wanukia, wa kiuchumi Tanzania,
Mambo yanaharibiwa, kwa wachache kutegemea,
Kisasi wanaotumia, dhidi ya wao wabaya,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

Watawala walokuwa, wataka kushangiliwa,
Hata wanapokosea,si ruksa kuzomea,
Na hili twalikataa,sio demkorasia,
Serikali kama wewe, iwezayo weza fanza!

No comments: