UNAJIFANYA kujua, kubisha na kukataa,
Hali wote wanajua, ilivyo yako tabia,
Hutena ukakosea, wengine kusingizia,
Lete sabau za msingi, sio msingi wa sababu!
Kwa kuwa ninakujua, sababu natarajia,
Uache kujitetea, ukweli kukubalia,
Ni wewe usiyejua, wengine wote wajua,
Lete sabau za msingi, sio msingi wa sababu!
Mzishi umeshakua, vyote vyenye manufaa,
Mwepesi kujitetea, kwa ujinga ulokuwa,
Na lawama kuzitia, usipate laumiwa,
Lete sabau za msingi, sio msingi wa sababu!
Kiumbe unapotea, muovu umeshakua,
Watu wanakushangaa, nini kimekuingia,
Au umeshachezewa, na wachawi walokua?
Lete sabau za msingi, sio msingi wa sababu!
Mahaoka ukiondoa, unaweza kurejea,
Si wewe uliyekuwa, hilo sasa natambua,
Nami ninakataa, ubaya kukutendea,
Lete sabau za msingi, sio msingi wa sababu!
Na umeshanitendea, na wewe unayajua,
Akili nazo ukiwa, hayo hautarudia,
Haraka utaridhia, nyumbani ukarejea,
Lete sabau za msingi, sio msingi wa sababu!
Sunday, March 4, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment