Tuesday, June 12, 2012

Ham, Shem na Jafeti

QURAN haitambui, wala  haijaisikia,
Nikaupata uhai, ukweli kuuchunugua,
Kumbe yote ni nishai, mkono  mtu katia,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Hizo zote simulizi, weusi kujichukia,
Na kuwa nayo mapenzi, na weupe usofaa,
Hali nao hawawezi, husuda imewajaa,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Kama ni kukata kuni, Mzungu sasa ridhaa,
Jahanamu duniani, kwa wengi imeingia,
Huko kwao maskani, shida zinawazidia,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Waarabu wauana, asubuhi na mchana,
Zimewazidi hiana, hakunao uungwana,
Syria ukiona, damu wanamimizana,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Mweusi kwa kuzubaa, mengi kasingiziwa,
Kalamu haikujua, lipi lake angetia,
Uongo katengezewa, hadi kuukubalia,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Ni ulozi ulokuwa, Mzungu kumtegemea,
Uoga ukamwingia, madaraka akitwaa,
Ila ninavyotambua, akili hatujatumia,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Ngono tumesingiziwa, ndio tuliolaniwa,
Na wazungu wamejaa, kwenye dini waitia,
Na sinema nazo pia, mitandao imejaa,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Nani aliyelaaniwa, Sodama waelekea,
Mwafrika kahofia, ila wale wenye njaa,
Na kama mnavyojua, ukafiri huja kwa njaa,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Mwafrika kajaliwa, kila kitu amepewa,
Na njia ya kumwingia, kujifanza unajua,
Ujinga ukamtia, wewe kukutegemea,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Maisha yamzingua, akataa kusinzia,
Kichwa kajitingishia, mapya kujamwingia,
Nje akiangalia, sinema ajionea,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Hata juu walokuwa, chini anawangojea,
Ajira sasa kutoa, Wazungu akatumia,
Angola yanatokea, Msumbiji nako pia,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Kwa Mzungu sasa njaa, zindukeni Tanzania,
Akili mkifukia, patupu kuambulia,
Kuamka mnatikiwa, Wazungu kuwatumia,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Bandari kujijengea, ajira kuwamwagia,
Na kazi wasiokuwa, Ulaya tele wamjeaa,
Mnalingoja bamvua, wenzi hawatachukua ?
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Reli imeishachaa,  mpya inatakiwa,
Wahandisi wamejaa, kazi wajitafutia,
Nyie ndani mmekaa, msada mwaungojea,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Barabara zinakiwa, kwa kushoto na kulia,
Wako tele injinia, ujenzi wanaujua,
Uongozi mwashangaa, mna akili za njaa ?
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

Ni ishirini na mbili, hivi sasa twaingia,
Mwajitia udhalili, kila kitu kununua ?
Kweli njaa ya akili, ndiyo iliyo balaa,
Ham, Sham na Jafeti, ni hadithi ya kaburu:
Kwenye biblia katia,
Kwa chuki iliyomjaa,
Mke kupenda mweusi !

No comments: