Saturday, June 2, 2012

Kweli wazaliwa nao



DAIMA usitegemee, hawa utakufa nao,
Watu uwasaidie, hata ndugu pia nao,
Na kisha uwaachie, waende na njia zao,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa kwao!

Mzaliwa hufi naye, hayo kwenye zama zao,
Sikuhzi tujigawe, kila mtu na makwao,
Na omab yakutokee, katika yako makao,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa nao!

Viumbe waangalie, njiani waangukao,
Bahati wakwangalie, waitambue haliyo,
Kisha tena ujaliwa, wawe ni wa kufaao,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa kwao!

Katu tusijichafue, misafi iwe mioyo,
Uyafanze kama wewe , usitende kama wao,
Huruma usiishiwe, ndiyo ikuokoayo,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa nao!

Viumbe uwatambue, ujana ni uwaponzao,
Wanawali waishiwe,  ikafa mioyo yao,
Ajuza achuchumae, sio vitini wakaao,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa nao!

Laana wasiitambue, kimya waipewayo,
Na vijana na wazee, msaada wautakao,
Nao wasijitambue, ila ni urembo wao,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa nao!

Hawa uwafumanie, uchungu wao ujao,
Manesi wawakimbie, kwenye hizo saa zao,
Msaaada wasipatiwe, na ndio wajifiao,
Kweli wazaliwa nao, nadra ukafa nao!


No comments: