Saturday, June 2, 2012

Mwalimu mwenye ajenda



Wanafunzi hatufai, mwenye ajenda binafsi,
Mwalimu mwenye nishai, elimuye wasiwasi,
Hata kama ni digrii, pengine ni kinamasi,
Mwalimu mwenye ajenda, binafsi hatufai !

Ni mtu wa kukinai, kama vile makamasi,
Si kwa  nazi wala tui, yalo yake wasiwasi,
Na hata ukimrai, haitambui nafusi,
Mwalimu mwenye ajenda, binafsi hatufai !

Mtu wa namna hii , ualimu anahasi,
Kumchagua jinai, ndani ana ibilisi,
Kitu chema hakizai, bali dhiki na maasi,
Mwalimu mwenye ajenda, binafsi hatufai !




No comments: