Tuesday, June 12, 2012

Wako wapi watu safi ?




Haiwi mjigawie, mkavila kwa ulafi,
Na kisha mtumainie, roho yangu kuwa safi,
Ni raia mnijue, kwa herufi na sarufi,
Wakowapi watu safi, nuksi waziondoe ?

Bure msinibague, mnifanze pamba fifi,
Yenu mjue, yngu msijue, kisha nipige makofi,
Huja yenu niachie, mkaukwaa msufi,
Wakowapi watu safi, nuksi waziondoe ?

Uongozi si tumbawe, za uchafu na usafi,
Watu msiwakimbie, wakawashinda masuffi,
Kwenye shida mkkakae, kwa dhiki mtu hafi,
Wakowapi watu safi, nuksi waziondoe ?

Wa chini mwanyanyue, hata kama wakorofi,
Uongozi ni mayowe, harufu zisizo safi,
Na kelele msikie, si bidhaa, mali ghafi,
Wakowapi watu safi, nuksi waziondoe ?

Msambe mkanambie, wa Mombasa na Kilifi,
Hino mkaziandae, kiasi chake ukufi,
Na ndima mnigawie, huo nd'o wetu ulafi,
Wakowapi watu safi, nuksi waziondoe ?

Ndwele ziwatatulie, kwa shemeji na mawifi,
Nyengine ziaguliwa, kwa kusoma zake shafi,
Neema iwatambue, heri ipige makofi,
Wakowapi watu safi, nuksi waziondoe ?



No comments: