Saturday, June 2, 2012

Eti ameshachanjiwa


ADAI keshachanjiwa, tena siku nyingi sana,
Kuukosa atwambia, hilo halitawezekana,
Mzizi keshachimbia, uani umeshabana,
Eti ameshachanjiwa, na hawezi kuukosa !

Mganga wamtambua, wakubwa pia mabwana,
Tunguri  huzitungua, asubuhi na mchana,
Na yao wanatambua,  kama siye kutofana,
Eti ameshachanjiwa, na hawezi kuukosa !

Umungu wamemtia, japa kashiba ubwana,
Na riziki atupiwa, kazi yake kujichana,
Maisha ajipatia, wamfaa muamana,
Eti ameshachanjiwa, na hawezi kuukosa !

Hawezi kuwaachia, lazima kushika sana,
Bila wao kuna njaa, ataaibika mchana,
Hatoweza kuwatishia, naye tena fungamana,
Eti ameshachanjiwa, na hawezi kuukosa !

No comments: