Saturday, June 2, 2012

Chemshakinywa hakuna

Baba yenu hela sina, ninaitwa Halahela,
Mnataka kujichana, niifanze gani hila,
Chemshakinywa hakuna, na mchana halahala,
Walilia chai wana, chemshakinywa hakuna !

Na mwenzenu kazi sina, na nchi haina jamala,
Maneno tupu wanena, hawajui hatujala,
Tena si tokea jana, ni juzi tulipokula,
Walilia chai wana, chemshakinywa hakuna !

Ukowapi muamuna, serikali na fadhila,
Njaa inapokubana, kila kitu mbona hela,
Hamnao waungwana, kuyaondoa madhila,
Walilia chai wana, chemshakinywa hakuna !

Wangekuwepo vijana, nje waliyoyalola,
Waneiffanza hisana, walatu tupate kula,
Na mengine kifanana, zingeshaondoka hila,
Walilia chai wana, chemshakinywa hakuna !

No comments: