Wednesday, December 14, 2011

Wasomi Wajiolojia

Ni wapi wameishia, wasomi wa jiologia,
Baba aliowandaa, na msingi kujengea,
Hivi hivi twapotea, na daftari lao pia?
Wasomi wajiolojia, wapi walipofukiwa?

Chuoni ni hapa Daa, kikuu waliangaliwa,
Hakika nilivyojua, kila kitu kuchimbua,
Wenyewe kujitegemea, na sio hii sanaa,
Wasomi wajiolojia, wapi walipofukiwa?

Paseni watu kupewa, mali wameziachia,
Kweli njaa ikizidia, mafuu mtu anakua,
Ndivy ilivyotokea, wenzetu kunajisiwa,
Wasomi wajiolojia, wapi walipofukiwa?

Kila nikiwaangalia, nashindwa kuwaelewa,
Akili zimepungua, au maradhi waugua,
Hawajui cha kufaa, na kile kisichowafaa,
Wasomi wajiolojia, wapi walipofukiwa?

Waachiaje kwa mamia, moja tu ukapokea,
Huku si kulaaniwa, au njaa kulogewa,
Haijawa nakataa, kuyaacha manufaa,
Wasomi wajiolojia, wapi walipofukiwa?

No comments: