Mtaja ahamanika, mganga amefariki,
Malengo aliyoweka, apaswa kuyahakiki,
Vigumu kuja kufika, kaondoka mshiriki,
Mganga akifariki, mteja huhangaika.
Ataka kutajirika, bilaye hatajiriki,
Ataka kuneemeka, pasiye haneemeki,
Ukubwa aliutaka, ni mbali sasa hafiki,
Mganga akifariki, mteja huhangaika.
Kaondoka mshirika, cheo hakieleweki,
Ni wapi atapashika, maisha yamuafiki,
Au aja kufutika, bila kuandikwa chaki?
Mganga akifariki, mteja huhangaika.
Mtaja ahangaika, mganga amefariki,
Ndoto imeshaondoka, safari haikamiliki,
Yamtatiza mashaka, amebaki kuhamaki,
Mganga akifariki, mteja huhangaika.
Thursday, December 1, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment