HIvi tumeshalaaniwa, au hatujajitambua,
Ni akili kumi kupewa, mabilioni yakapaa?
Au kujajitegemea, wenyewe kujivunia?
Akili kupewa kumi, milioni kutwaliwa?
Mzaliwa ninalia, haya ninajionea,
Laiti ningelitambua, hivi nisingezaliwa,
Rangi ningechagua, nyeusi isiyokua,
Akili kupewa kumi, milioni kutwaliwa?
Unafiki watujaa, dhuluma twajitetea,
Mola atushangaa, kuthubutu kuhadaa,
Ila naye namjua, muda anaungojea,
Akili kupewa kumi, milioni kutwaliwa?
Kiburi kikichanua, hasira zake hujaa,
Ndipo anapoamua, wanafiki kuumbua,
Mchana tena ikawa, wote tunashuhudia,
Akili kupewa kumi, milioni kutwaliwa?
Wednesday, December 14, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment