Saturday, December 29, 2012

Pepo walokwishapewa



WAMEKWISHACHAGULIWA, vitini wameshakaa,
Japo katika dunia, bado wanaendelea,
Lakini na huko pia, wamekwishaingia,
Pepo walokwishapewa, ndio wataonilipa !

Na katika mazulia, jina watajionea,
Nao wakalinyanyua, na kitini kulitia,
Na wajapo kuuliziwa, wao wataitikia,
Pepo walokwishapewa, ndio wataonilipa !

Wataitikia radhia, na yeye yu nasi pia,
Haitotimu wakiah, na mimi nitaingia,
Milizamu nimejaa, majoho kinyunyizia,
Pepo walokwishapewa, ndio wataonilipa !

Milizamu nimejaa, majoho kinyunyizia,
Ya fahari na furaha, na mimi kufikiriwa,
Heshima kubwa kupewa, kwenye zama nilokuwa,
Pepo walokwishapewa, ndio wataonilipa !

Sharifu kushuhudia, Modhari mtangulia,
Baraka aliyotoa, bure kumbe haikuwa,
Heshima niloigawa, leo inanirudia,
Pepo walokwishapewa, ndio wataonilipa !

No comments: