Saturday, December 29, 2012

N A M B A



Anza na sifuri saba, kisha tano utatia,
Mbili ukiongezea, nane kuu kuanzia,
Sifuri ikafatia, kisha nane kurejea,
Likizo ninapokuwa, unaweza nipigia ?

Bado hatujamilizia, takwimu yaendelea,
Tano ukaendelea, tatu ikafatia,
Kisha utamalizia, kwa tisa kuitumia,
Likizo ninapokuwa, unaweza nipigia ?

Hapo utapokelewa, kwangu kuelekezewa,
Rahisi haitakuwa, na mimi kuongea,
Ila wapo maridhia, ujumbe watapokea,
Likizo ninapokuwa, unaweza nipigia ?

Facebook kiingia, waweza ujumbe tia,
Hapo nitajisomea, majibu nikayatoa,
Muda yaweza chukua, Kijijini ninapokuwa,
Likizo ninapokuwa, unaweza nipigia ?

Twitter nimefungua, pia waweza tumia,
Ukishaniandikia, ujumbe nitatumiwa,
Mie nikijisomea, majibu sintoshelewa,
Likizo ninapokuwa, unaweza nipigia ?



No comments: