Saturday, December 29, 2012

Karibu kwenye dunia yangu.



Karibu kwangu  nyumbani
Nikiamini yakini
Je, hauingii ndani
Maajabu hutokea
Ingawa kwa nadra!

Ingia mwangu moyoni
Tupa mbali yako huzuni
Karibu kwenye dunia yangu
Kama vile ni mwenzangu !

Piga hodi
Utafunguliwa....
Tafuta
Na utapata
Ulizia
Na utaupewa
Ufunguo wa moyoni kwangu

Nitakuwa ninasubiri hapa
Mikono yangu ikiwa wazi
Nikikusubiri wewe tu
Karibu kwenye dunia yangu...
Kwa kuniunga mkono, sintocha kukupenda !



No comments: