Tuesday, December 11, 2012

Hapajawa wa mkubwa


UBINAFSI walojaa, wa kwako watamlea,
Wa kwao waanglia, si wenu kusaidia,
Nafusi wamefulia, hasadi kwa kuwajaa,
Hapajawa wa mkubwa, vipaji watavilea?

Ukubwa kwao ni njaa, yao tu kujigangia,
Mengine huyakimbia, wenyewe kuwaachia,
Na michezo nayo pia, vivyo hivyo itakuwa,
Hapajawa wa mkubwa, vipaji watavilea?

Ubepari kuuzua, haya walikijayua,
Wao juu watakwaa, uongozi kununua,
Urishi ukishajaa, wana watawaachia,
Hapajawa wa mkubwa, vipaji watavilea?

Ufisadi ukikua, wana watajipatia,
Yao yakaendelea, vitini wakijitoa,
Dhiki wataikimbia, na siasa za balaa,
Hapajawa wa mkubwa, vipaji watavilea?

Kwao watajichimbia, kula walivyojaliwa,
Uchoyo kuendelea, hadi gizani ikawa,
Nani wa kuwumbua, na shibe waitumbua?
Hapajawa wa mkubwa, vipaji watavilea?


No comments: