MZIGO nilochukua, uzito wanizidia,
Ni mashaka imekua, nitakapo kuutua,
Kila nikikusudia, mzigo unakataa,
Mzigo niliotwaa, ninashindwa kuutua!
Maarifa umejaa, kasha nililolitwaa,
Mtu utalidhania, kwa ninavyofikiria,
Ukibeba hulegea, jepesi ukadhania,
Mzigo niliotwaa, ninashindwa kuutua!
Ila ukikusudia, kichwani kulioindoa,
Daima hukakamaa, kama maiti likawa,
Mwishoni hujiachia, liendelee kukaa,
Mzigo niliotwaa, ninashindwa kuutua!
Washairi mwasikia, zigo linavolemea,
Sijui kama mwajua, jina linaloufaa,
Na dawa kuniambia, ya kuja kuliondoa,
Mzigo niliotwaa, ninashindwa kuutua!
Wednesday, January 4, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment