Umeme tatizo mjini
Sio letu vijijini
Ni miaka hamsini
Tungali hatuuoni
Ikishafika jioni
Tu kama kuku ni ndani
Vitabu bure thamani
Atakayesoma nani
Totoro humo gizani ?
Wapenzi hawaonani
Bila vijinga mkononi,
Mlo ukishauwini
Huitwa usingizini
Matokeo mwabaini
Makinda wa vijijini
Kwa wingi tuna nishani
Ila kwa hali taabani!
Nauwaza usononi
Na matamko kinywani
Sio laana yakini
Watulani vijijini
Yatukutayo mjini
Si bure ninaamini!!!
Wednesday, January 4, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment