Wednesday, January 4, 2012

Huona upweke bora

Itakupata hasara, nawe usiposowera,
Nyingine bandia sura, au mtu kajichora,
Huwa kukuru kakara, kuona ya kweli sura,
Huona upweke bora, kuliko za mgando sura!

Wanawali ni majura, asili wanaichokora,
Ya kwao wanayagura, wafata yaso tijara,
Tazama kina Ashura, mchana wanavyong'ara,
Huona upweke bora, kuliko sura hadaa!

Wafaulu kujipara, kuitafuta ajira,
Waupatao mshahara, yasiyokwisha madhara,
Uzeeni hudorora, upinde zikawa sura,
Huona upweke bora, sura za kuchuna mbaya!

No comments: