Thursday, January 5, 2012

Mlenda

Ili mradi wasunda, athari huvumilia,
Wanaopenda mlenda, mnato wanaujua,
Hauachi kukuganda, mkono ukishatia,
Mlenda ukiupenda, kamasi utakataa?

Ni kiuno na mkanda, mlenda nacho kinyaa,
Ladha yake ni udenda, kooni ukiutia,
Na bada ukilidunda, ngoma chini hutulia,
Mlenda ukiupenda, kamasi utakataa?

Huumeza kwa mafunda, mkono bila tulia,
Kama pete nake chanda, hufanza wake ubia,
Tumboni unayotenda, raha tupu husikia,
Mlenda ukiupenda, kamasi utakataa?

Mnyaramba nampenda, mlenda anaujua,
Sintoacha kumdanda, njaa ninaposikia,
Nitabeba na matunda, kwenda kumzawadia,
Mlenda ukiupenda, kamasi utakataa?

No comments: