Thursday, November 8, 2012

Watani wa maisha




Katibani naingia, hoja yanguu kuitoa,

Wazee kuamkia, vijana kusalimia,

Miaka imefikia, kijana kumchagua,

Wastani wa maisha, ni miaka hamsini;

Rais wa Tanzania, asizidi wastani:

Mtu hatujamchulia !



Rais anatakiwa, arobaini akiwa,

Uzee akiingia, hamsini kuishia,

Kumi akihudumia, sitini kuifikia,

Msiambe sikuyateta

Wastani wa maisha, ni miaka hamsini;

Rais wa Tanzania, asizidi wastani:

Mtu hatujamchulia !



Hamsini walozaliwa, ukingo wamefikia,

Hadithini kuishia, waende kusimulia,

Sasa wanaotakiwa, sitini walozaliwa,

Wastani wa maisha, ni miaka hamsini;

Rais wa Tanzania, asizidi wastani:

Mtu hatujamchulia !



Na sabini wanafaa, sifa wakishajaliwa,

Hao watayaelewa, ya vijana Tanzania,

Wengine wawahadaa, wenyewe kwenda jifaa,

Wastani wa maisha, ni miaka hamsini;

Rais wa Tanzania, asizidi wastani:

Mtu hatujamchulia !

No comments: