Friday, November 2, 2012

Ndizi ni wetu mwokozi

KIlimo chetu katizi, mvua hazimalizi,

Hali ya hewa yaizi, vilivyo na mazoezi,

Mahindi navyo viazi, kuota sasa ni kazi,

Ndizi ni wetu mwokozi, njaa haina ajizi.

Kilimo wake watunzi, wanapendekeza ndizi,

Tuoteshe wanagenzi, na kuzipa matanuzi,

Itakuwa ni mwokozi, huko mbele ya miezi,

Ndizi ni wetu mwokozi, njaa haina ajizi.

Hali hamjiulizi, muionayo makazi,

Mchele una ajizi, bei unapanda ngazi,

Na unga wa sikuhizi, njaa hauimalizi,

Ndizi ni wetu mwokozi, njaa haina ajizi.

Umebaki utatuzi, raia pandeni ndizi,

Hata katika majenzi, na mahala penye kazi,

Ndizi kesho ni mlezi, njaa isiwe uchizi,

Ndizi ni wetu mwokozi, njaa haina ajizi.

No comments: