Thursday, November 8, 2012

Hudanganywa kwa shilingi

UZIMA uliyepewa, shilingi ya kununua ?

Mtu akakutumia, kama bidhaa ukawa,

Haya kutojionea, na kesho kutohofia ?

Hudanganywa kwa shilingi, watu wajinga wakawa !

Shilingi kweli maua, tena moyo inaua,

Aibu ikaitoa, haya mbali kuulia,

Mtu akaabudiwa, muumba asiyekuwa,

Hudanganywa kwa shilingi, watu wajinga wakawa !

Mushiriki kwenda kuwa, kiumbe akalaniwa,

Akaikosa janaa, na kupoteza dunia,

Na roho akitolewa, abaki kujijutia,

Hudanganywa kwa shilingi, watu wajinga wakawa !

No comments: