Thursday, November 8, 2012

Kisomali

Watushinda Somalia, Kisomali kuringia !

Sisi wa kutojijua, Kiswahili twalegea,

Siwezi kuja shangaa, nyuma tusipobakia,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Dalingi inshakuwa, ya kwao waitumia,

Waziri namsikia, nje ameteuliwa,

Chao anakiongea, jambo ung'eng'e ajua,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Utabiri nautoa, Somalia kwelekea,

Matata wakijivua, wataanza kuchipua,

Mola amewajalia, katikati wamekaa,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Mola amewajalia, katikati wamekuwa,

Kwa haiba wavutia, lugha rahisi kujua,

Wao wamedhamiria, ya kwao kujifanzia,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Lugha weataitumia, umoja kujiundia,

Kisha wakajichambua, wakajipanga upya,

Kuzingira tasnia, waweze kujinynyua,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Ndguu zao wamejaa, katika hii dunia,

Biashara wanajua, nyumbani watarejea,

Kwa lugha kupalilia, jamii wakanyanyua,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Mudha haitachuka, Kisomali kitakuwa,

Masomo kutafsiria, kwa lugha yao kutia,

Zipo teknolojia, rahisi haya yakawa

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

Ung'eng'e tuliolewa, kaeni kuangalia,

Inapaa Somalia, muda haitachuku,a

Nyie mlietangulia, wa mwisho mwaja mkawa,

Kwa kuenzi Kisomali, Somali kutangulia !

No comments: