Thursday, November 8, 2012

AZANI MSWALIHINA





Tabia tunamjua, haya asiyejaliwa,

Udhu akiichukua, afikiria zinaa,

Na sala anapotia, udenda unamjaa,

Anaposali azani, hubakia malaika?



Mola ninamuombea, kiumbe aliyepagawa,

Pepo asijekataa, kwa kutobadili tabia,

Akachochea mkaa, wa kwenda kesho kukaa,

Anaposali azani, hubakia malaika?



Huruma namuoneya, kiumbe asojijua,

Pepo amemuingia, kama njia kumtumia,

Maovu ahudumia, aje kesho kuungua,

Anaposali azani, hubakia malaika?



Mtegoni awatia, wengi wasiojijua,

Kibiriti kikitiwa, wote wanauchukua,

Kilio tutasikia, inshallah siku ikiwa,

Anaposali azani, hubakia malaika?



No comments: